Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, amesema kuwa hakuna sababu yoyote wala mipaka ya kijiografia inayoweza kuvunja uhusiano wa kindugu na wa kihistoria uliopo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea hati za utambulisho za Balozi mpya wa Iraq nchini Iran, Yasser Abdulzahra al-Hajjaj, Pezeshkian alimtakia mafanikio katika kipindi chake cha uwakilishi wa kidiplomasia na kusisitiza kuwa uhusiano kati ya Iran na Iraq una mizizi ya kina.

Alisema kuwa mahusiano ya mataifa hayo mawili yanazidi uhusiano wa kawaida wa nchi jirani, kwani yamejengwa juu ya msingi wa historia, utamaduni, dini na ustaarabu wa pamoja.

Rais Pezeshkian aliongeza kuwa wananchi wa Iran na Iraq wanashirikiana hatima moja, maslahi ya pamoja na malengo yanayofanana, akisisitiza kwamba uhusiano huo wa kindugu ni imara kiasi kwamba hakuna sababu yoyote wala mipaka inayoweza kuuvunja.

Dakta Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa, uhusiano kati ya Iran na Iraq unazidi ule wa kawaida wa nchi jirani, kwani umejengwa juu ya misingi ya kina ya historia, utamaduni, dini na ustaarabu wa pamoja.

Rais Pezeshkian amesema mataifa hayo mawili yanapaswa kuimarisha ushirikiano katika nyanja zote, ili kuendeleza mshikamano wa kikanda na kutumia ipasavyo fursa na uwezo wa pamoja uliopo.

Ameongeza kuwa kuimarishwa kwa ushirikiano huo kutachangia kufikiwa kwa amani, usalama, ustawi wa wananchi na maendeleo endelevu katika eneo la Asia Magharibi.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa ushiriki mkubwa wa wananchi wa Iraq katika shughuli za mazishi ya kihistoria ya Kiongozi Shahidi wa Iran ni ishara ya wazi ya uhusiano wa kina wa kihisia, kiitikadi na kiutamaduni kati ya mataifa ya Iran na Iraq.

Amesema mahudhurio hayo makubwa na ya kipekee yalikuwa jambo ambalo wachambuzi wengi na mataifa ya kigeni hawakutarajia, na kwamba yameonyesha wazi kuwa mtaji wa kijamii uliopo kati ya wananchi wa Iran na Iraq ni hazina isiyo na mfano katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kuendeleza mshikamano wa kikanda.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *