Nchini Kenya, mpango wa kufungua kituo cha karantini kwa raia wa Marekani walioathiriwa na virusi vya Ebola kinakabiliwa na vita vya kisheria na kisiasa.Kituo hiki ambacho kilipangwa kufunguliwa katika kambi ya anga ya Laikipia katikati mwa nchi, kilifichuliwa na vyombo vya habari vya Marekani mwezi Mei. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Albane Thirouard

Kesi hiyo ilizua ghadhabu nchini Kenya, wakati maandamano yalifanyika siku kadhaa, ingawa nchi hiyo haijarekodi visa vyovyote vya virusi hivyo. Kufuatia pingamizi la kisheria lililowasilishwa na shirika moja, mahakama ilisitsha mradi huo ikisubiri uamuzi kuhusu uhalali wake. Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa Novemba 26, huku awamu ya kusikiliza kesi ikiwa imekamilika.

Hoja hizo ziliwasilishwa siku ya Alhamisi, Julai 23, na Ijumaa, Julai 24, 2026, mbele ya Mahakama Kuu jijini Nairobi. Walalamikaji wanalaani mradi uliofanywa bila kushauriana na taasisi husika na ambao wanadai unahatarisha maisha ya raia. Kulingana na walalamikaji, Kenya haina vifaa vya kutosha kukabiliana na virusi vya Ebola.

Kwa upande wao, mamlaka, kupitia mawakili wao, wanasisitiza kwamba wamefuata sheria. Wanatetea mradi ambao, kulingana nao, ni sehemu ya mkakati wa kuzuia maambukizi ya virusi vya Ebola.

Tukisubiri hukumu inayotarajiwa mwezi Novemba, hatua ya kusitishwa kwa mradi huo bado kunaendelea. Hatu hiyo nakataza uendeshaji wa kituo kilichopangwa cha karantini huko Laikipia.

Karantini tayari zinaendelea nchini Kenya

Licha ya kusitishwa kwa mradi huo, shirika lisilo la kiserikali la Marekani lilitangaza wiki iliyopita kwamba wanachama saba wa timu yake walikuwa karantini nchini Kenya baada ya kushiriki katika zoezi la kukabiliana na Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Washington ilithibitisha uhamisho wa raia wake kadhaa hadi kituo kinachoendeshwa na wafanyakazi wa Marekani nchini Kenya, baada ya idhini kutoka Nairobi. Hata hivyo, mamlaka ya Marekani haikutaja eneo halisi la kituo hiki.

Ikiwa watu hawa walihamishwa chini ya makubaliano yaliyopingwa mahakamani, “itakuwa kashfa kubwa,” limesema shirika lisilo la kiserikali la Katiba Institute, ambalo liliwasilisha kesi hiyo mahakamani. Waziri wa Afya, kwa upande wake, anabainisha kwamba ameheshimu uamuzi wa Mahakama wa kusitishwa kwa mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *