#HABARI: Tayari Uganda imetoa idhini ya awali kufuatia ombi la moja kwa moja kutoka kwa Rais wa Marekani, Donald Trump hadi kwa Rais Yoweri Museveni.
Inasemekana Rais Trump aliiomba Uganda kuunga mkono kuanzishwa kwa kikosi cha kimataifa nchini Gaza kitakacholenga kukomesha machafuko, kulinda raia, na kuharakisha utoaji wa misaada ya kibinadamu pamoja na juhudi za ujenzi upya.
Afisa wa Israel alisema Baraza la mawaziri la usalama la Netanyahu, lilipitisha mfumo wa kisheria utakaoruhusu kikosi hicho kuingia Gaza huku Netanyahu akitarajiwa kuondoka kuelekea Washington siku ya Jumatatu na kukutana na Rais Trump siku ya Jumanne.
Afisa huyo alisema hicho kitakuwa Kikosi cha Kimataifa cha Uimarishaji wa Usalama (International Stabilization Force), kitakachohusisha wanachama 200 kutoka nchi “rafiki” ambazo ni pamoja na Morocco, watakaopelekwa katika maeneo ambayo hayako chini ya udhibiti wa Israel. Nchi husika zitahitajika kupata idhini ya Israel kabla ya kuruhusiwa kuingia Gaza.
Sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza bado imeharibika vibaya kutokana na miaka miwili ya vita vilivyochochewa na mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, 2023.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)