Bodi ya Amani itaundwa na viongozi wa dunia, na awali ilibuniwa kama sehemu ya mpango wa kujenga upya Gaza, lakini mamlaka yake yamepanuka.
Siku ya Jumatano, nchi saba zikiwemo Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na Misri zilitangaza kujiunga na bodi hiyo.
Israel pia imethibitisha hadharani ushiriki wake.
Idadi ya nchi zilikuwa tayari zimejiandikisha – ikiwa ni pamoja na Morocco, Belarus na Bahrain.
Canada, Urusi na Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yamealikwa pia.
Leo asubuhi Waziri wa Mambo ya Nje Yvette Cooper aliiambia BBC kwamba Uingereza haitatia saini leo, akielezea wasiwasi kuhusu kuhusika kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Trump ndio ameanza kuongea katika kongamano hilo linaloendelea kwasasa.
Anaiita “siku ya kusisimua sana, ndefu katika kutengeneza”. Anadai “kila mtu” anataka kuwa sehemu ya Bodi yake ya Amani.
Anasema ataendelea “kufanya kazi na wengine wengi, ukiwemo Umoja wa Mataifa”.
#chanzoBBCSWAHILI
#starTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)