Nchini Nigeria, ubomoaji wa kikatili wa makazi duni maarufu ya Makoko huko Lagos umeshtumiwa na mashirika ya kiraia. Makumi, labda hata mamia, ya maelfu ya watu wanaaminika kupoteza nyumba zao tangu kuanza kwa shughuli hizi za ubomoaji wa mazi mnamo mwezi Desemba. Ikituhumiwa kutenda nje ya mfumo wowote wa kisheria, serikali ya Jimbo la Lagos inasisitiza kwamba hii si “operesheni ya adhabu” wala mradi wa “kupambana na umaskini”.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Abuja, Liza Fabbian

Kutoka Daraja la Third Mainland Bridg, jamii ya Makoko inazidi kufanana na uwanja wa magofu yanayofuka moshi. Katika wiki za hivi karibuni, tingatinga, zikisindikizwa na jeshi, zimeharibu nyumba za mbao za eneo hilo la Lagos na kusababisha wakazi kutoroka eneo hilo.

Wengi wa wavuvi hawa sasa wanalala kwenye boti zao kwenye ziwa, wakiwa na mali chache walizoweza kuokoa. Jamii zingine zisizo rasmi katika eneo linalozunguka zimeharibiwa makazi yao kikatili vile vile: Oworonshoki, Owode Onirin, Otumara, na Baba-Ijora. Mashirika ya kiraia yanalaani mbinu za kikatili za mamlaka. Wakazi walifukuzwa kwa gesi ya machozi na risasi za moto. Watu kadhaa wanaripotiwa kupoteza maisha.

Ubomoaji bila mpango wa kuhamisha watu

Kimsingi, serikali ya Jimbo la Lagos inatetea vitendo vyake, ambavyo vinalenga kulinda ufuo wa maji kwa kuwazuia wakazi kukaa ndani ya mita 100 kutoka kwa nyaya za umeme zenye volteji nyingi zinazopakana na eneo hilo. Lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yanalaani ubomoaji unaozidi kikomo hiki na ulifanywa bila onyo la wazi na bila mpango wowote wa kuhamisha watu, huku mamlaka ikishutumiwa kutaka kunyakua ardhi hii ili kujenga vitongoji vipya vya makazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *