Chanzo cha picha, Getty Images
Umati wa
watu umekusanyika Minneapolis, Marekani kupinga uwepo wa maafisa wa
uhamiaji wa shirikisho katika jimbo hilo, baada ya kupigwa risasi na kuuawa Alex
Pretti mwenye umri wa miaka 37.
Gavana wa
Minnesota Tim Walz ametoa wito kwa Rais wa Marekani, Donald Trump
kuwaondoa maafisa hao wa shirikisho katika jimbo lake, akisema: “Huu
ni wakati wa mabadiliko.”
Katika
chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social, Rais wa Marekani Donald
Trump amesema Walz na Meya wa Minneapolis Jacob Frey wanapaswa kuwasalimisha “wahamiaji
wote haramu wahalifu” waliofungwa katika magereza ya serikali kwa
ajili ya kuwafukuza nchini.
Maafisa wa jimbo
na shirikisho wametoa maelezo yanayokinzana kuhusu tukio la kifo cha
Pretti siku ya Jumamosi.
Alipoulizwa
kuhusu video zilizoibuka zikionyesha tukio hilo la mauaji, Kamanda wa Doria ya
Mpakani Greg Bovino anasema kuna haja ya kuwepo kwa uchunguzi ili
kubaini ukweli.
Pia unaweza kusoma: