Nchini Uganda, vita mpya ya maneno imezuka kwenye mitandao ya kijamii kati ya mkuu wa jeshi na kiongozi wa upinzani Bobi Wine. Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais Yoweri Museveni, anakanusha kushambuliwa kwa mke wa Bobi Wine, Barbara Kyagulanyi, anayejulikana zaidi kama “Barbie.”  

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa upinzani—akiwa mafichoni kwa siku kadhaa baada ya uvamizi nyumbani kwake—anawashutumu wanajeshi kwa kumshambulia mkewe, ambaye kwa sasa amelazwa hospitalini. Upinzani unalaani kuongezeka kwa ukandamizaji, ulioambatana na maadhimisho ya miaka 40 ya Yoweri Museveni madarakani, Jumatatu, Januari 26.

Kwenye mtandao wa kijamii wa X, Muhoozi Kainerugaba anadai kwamba “askari wake hawakumpiga Barbie,” kabla ya kuongeza, “Hatuwapigi wanawake,” huku akidai kuwa wanamtafuta Bobi Wine, ambaye anamwita “mwoga.”

Bobi Wine anakanusha kinyume chake. Kulingana naye, wanajeshi waliingia kwa nguvu nyumbani kwao usiku wa Ijumaa, Januari 24, wakamnyonga na kumtukana mkewe, kisha wakaiba vitu vyote ndani ya nyumba.

Barbie anasema alikataa kufungua simu yake licha ya kuamriwa kufanya hivyo, kabla ya kutendewa vibaya. Tangu wakati huo amelazwa hospitalini mjini Kampala.

Tukio hili limefufua mvutano uliokuwa ukiongezeka wa siku za hivi karibuni. Muhoozi Kainerugaba, ambaye mara nyingi huelezewa kama mrithi anayedhaniwa kuwa wa Yoweri Museveni, hivi karibuni alichapisha—na kisha akafuta—ujumbe unataja kifo cha Bobi Wine.

Waziri wa Habari Chris Baryomunsi anabainisha kwamba Bobi Wine “hana sababu ya kujificha” na anahalalisha hatua ya kutuma vikosi vya usalama kuzigira nyumba yake,  ili kufuatilia watu “wanaokuja na kuondoka.”

“Kauli zisio kuwa na msingi”

Akiwasiliana na RFI, Joel Ssenyonyi, msemaji wa chama cha upinzani cha NUP, amelaani “mateso” hayo na kuchukulia kauli hizo kwamba hazina msingi.

“Kwa upande mmoja, wanadai kwamba hakuna mtu anayemfuata, na kisha, saa chache baadaye, jeshi linavamia nyumba yake, linampiga mkewe, na kuiba vitu vyote ndani ya nyumba. Kwa hivyo lengo la operesheni hii ni nini? Muhoozi, mtotowa Museveni na mkuu wa jeshi, alikuwa tayari amesema, ‘Hatumtafuti,’ na sasa anasema, ‘Hatukumshambulia mkewe, lakini tunamtafuta mumewe.’ Na Muhoozi huyu huyu amemtishia Bobi Wine mara kwa mara. Hata alizungumzia kuhusu kumuua. Kwa kuzingatia msimamo wake, hili si jambo la kuchukuliwa kirahisi.” Ndiyo maana Bobi Wine na mkewe wamejificha. Utawala unawafuata waziwazi. Museveni ametawala kwa mkono wa chuma kwa miaka 40. Anakandamiza upinzani, anawatendea kikatili wakosoaji wake—wengi wameuawa, wengi wako gerezani—na alidai asilimia 71 ya kura katika uchaguzi uliopita. Lakini tunajiuliza: ikiwa wewe ni maarufu sana, kwa nini uwatese wapinzani wako? Tunalengwa, na hata hatuelewi ni kwa nini,” anasema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *