Nigeria itawahukumu wanajeshi walioshtakiwa kwa jaribio la mapinduzi. Tangazo hilo limetolewa siku ya Jumatatu, Januari 26, na jeshi la Nigeria. Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliyopita, wanajeshi 16 walikamatwa, rasmi kwa “utovu wa nidhamu.” Uvumi wa jaribio la mapinduzi, uliosambaa kwenye vyombo vya habari, ulikanuswa rasmi. Kwa hivyo, kwa kutangaza kesi hii ijayo, Lagos inakubali kuwepo kwa njama hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Uchunguzi kuhusu jambo hili umekamilika,” amesema msemaji wa jeshi la Nigeria. Imewaruhusu “kutambua maafisa kadhaa wanaoshukiwa kupanga njama ya kuipindua serikali.” Wale wanaoshukiwa “watafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi.”

Taarifa rasmi haionyeshi tarehe ya kesi hiyo, wala idadi ya wanajeshi watakaofikiswa mahakamani. Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliyopita, maafisa kumi na sita walikamatwa. Sababu rasmi iliyotolewa wakati huo ilikuwa “masuala ya nidhamu.”

Haijulikani kama kuna askari yeyote aliyekamatwa ambaye alifutiwa mashtaka au kama watu kadhaa wapya walikamatwa tangu wakati huo.

Miezi mitatu iliyopita, Rais wa Nigeria Bola Tinubu alikana kuwepo kwa jaribio lolote la mapinduzi, lakini alifanya mabadiliko makubwa ndani ya jeshi. Jenerali Christopher Musa, ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa jeshi, alikuwa miongoni mwa wale waliofukuzwa kazi kabla ya kurejeshwa kazini na kuteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi mwezi Desemba.

Kwa zaidi ya muongo mmoja, jeshi la Nigeria limekuwa likishiriki katika vita kali ya kupambana na ugaidi dhidi ya wanajihadi wa Boko Haram na washirika wa ndani wa kundi la Islamic State kaskazini mashariki mwa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *