#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali imefanikiwa kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu, wanaoingia nchini baada ya Idara ya Uhamiaji kufunga jumla ya vipenyo 1,777 vilivyokuwa vinatumika kuingia nchini kwa njia zisizo halali.

Waziri Katambi ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Jijini Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, pamoja na kudhibiti uhalifu unaochangiwa na uingiaji wa raia wa kigeni bila kufuata taratibu za kisheria.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *