‎#HABARI: Mwanaume mmoja aliyekuwa akisafirisha gari la IT amefariki dunia kufuatia ajali ya kugongana uso kwa uso na lori la mafuta katika eneo la Nane Nane, Manispaa ya Morogoro.

Tukio hilo lilitokea Januari 31, 2026, majira ya saa mbili usiku likihusisha magari zaidi ya moja katika barabara kuu ya Morogoro–Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, chanzo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva wa gari ndogo aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine yaliyokuwa kwenye foleni.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Nasoro Matua, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku juhudi za uokoaji zikifanyika mara baada ya tukio.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *