#HABARI: Mashabiki wa klabu ya Esperance De Tunis kutoka Tunisia wameeleza kuridhishwa kwao na huduma za Reli ya Kisasa (SGR), wakisema imewawezesha kusafiri kwa urahisi na kufurahia utalii nchini Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Stesheni ya SGR Magufuli Jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Morogoro, shabiki wa Esperance De Tunis, Aziz Hatur, amesema safari yao ya kutumia SGR kwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi imekuwa salama, ya kufurahisha na yenye huduma bora.
Aziz amesema kundi lao (Mashabiki) lilifanya safari mbili kwa kutumia SGR, safari ya kwanza ikiwa ni siku ya kwenda Morogoro na ya pili siku ya kurudi Dar es Salaam, na zote zilifanyika kwa viwango na mafanikio makubwa.
Amesema kuwa, safari hiyo ya kitalii imewawezesha kuona vivutio vya utalii kwa muda mfupi huku wakifurahia ubora wa huduma zinazotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), akibainisha kuwa yeye binafsi na kundi zima la mashabiki walifurahia safari hiyo.
Kutokana na uzoefu huo, Aziz amewahimiza Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi kutumia huduma za SGR, akisema ni njia salama na ya kuaminika ya usafiri, hasa kwa safari za kitalii.
Mashabiki hao wa Esperance De Tunis walitumia fursa ya uwepo wao nchini kutembelea vivutio vya utalii, wakati wakisubiri mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC, unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo Jumapili Februari Mosi, 2026.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.