
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ) imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kushiriki katika maandamano ya hasira na shughuli za mashinikizo dhidi ya mashambulizi na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Taarifa iliyotolewa na Hamas imesema kwamba “mashambulizi ya kikatili yanaoendelea kufanywa na utawala vamizi na wa kifashisti dhidi ya watu wetu huko Gaza, kupitia kuzidisha mashambulizi ya kinyama na kufanya uhalifu mkubwa zaidi wa kimfumo wa mauaji, kwa kulipua na kuharibu mahema na nyumba za raia wasio na hatia wala ulinzi, yanaonyesha azma ya utawala huo ya kuendeleza uhalifu mbaya zaidi wa kimfumo wa mauaji na kuongeza mateso ya wanadamu katika eneo hili la Palestina.”
Hamas imeongeza kuwa “serikali ya mhalifu wa kivita, Benjamin Netanyahu, inaendelea kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kila siku na kwa makusudi, ikikwepa majukumu yake kwa wapatanishi, kupuuza sheria na kanuni za kimataifa, na kukiukaji waziwazi maadili na kanuni zote za kibinadamu.”
Taarifa hiyo imesema: “Tunaelekeza wito kwa watu wenye dhamiri na watu huru katika Umma wa Kiarabu na Kiislamu na dunia nzima, kuchukua hatua za haraka za kushiriki katika za maandamano ya kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza na kuunga mkono mapambano yetu ya kiadilifu, katika miji mbalimbali, miji mikuu na maeneo tofauti kote ulimwenguni, dhidi ya ukatili usio wa haki wa utawala vamizi na wa kifashisti wa Israel.”
Hamas imesema, “Siku zijazo, hasa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ya kila wiki, ziwe harakati endelevu duniani inayoakisi sauti ya dhamiri ya kimataifa na kilio chake cha kupigania uhuru dhidi ya utawala vamizi, uchokozi na mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza.” Hamas ikewataka walimwengu kuuwekea mashinikizo utawala haramu wa Israel ili usimamishe mashambulizi yake ya kikatili, kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano, na kuanza mara moja kufungua vivuko vya mpakani na ujenzi upya wa Gaza.”
Israel inatataka kuwafukuza Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na tangu kuanza kwa muhula wa pili wa Rais wa Marekani Donald Trump Januari 2025, alitoa pendekezo la kuwahamisha Wapalestina hao na kuwapeleka Misri na Jordan, pendekezo ambalo limelipingwa vikali na Cairo na Amma.