#HABARI: Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania Mhe. Abdallah Ulega amesema katika kipindi cha siku 100 za awali za Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mwezi Novemba, Disemba na Januari 2026, wamepokea jumla ya shilingi Bilioni 511 kwa ajili ya kulipa madeni ya Makandarasi waliotekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi nchini Tanzania.

Akizungumza leo Jumapili Februari 08, 2026 Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wakati akieleza mafanikio katika sekta ya ujenzi kwenye siku 100 za awali za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika awamu yake ya pili ya Uongozi, Waziri Ulega amesema kati ya fedha hizo Bilioni 280 zimetoka hazina na zilizosalia zimetoka katika miradi ya wafadhili wa miradi ya ujenzi.

“Kati ya hizi Bilioni 280 za hazina, Bilioni 125, zimetoka kwenye mfuko wa barabara na zimelipa wakandarasi wadogo wazawa wanaotekeleza miradi ya ujenzi.” Amesisitiza Waziri Ulega.

Katika hatua nyingine, Ulega amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kufanya maboresho ya kimuundo na kiutawala kwa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ili kuongeza ufanisi na udhibiti wa fedha za umma suala ambalo liliifanya TEMESA kushindwa kulipa madeni.

Waziri Ulega amesema kwasasa wamechukua hatua zaidi za kuboresha Uongozi wa wakala huo, akisisitiza kuwa kuwapo kwa usimamizi na mifumo sahihi katika Wakala huo kutawezesha ulipaji wa madeni yanayodaiwa kwa Wakala huo, akisema uongozi uliokuwepo ulisababisha pia ubadhirifu wa fedha kutokana na kuwa na watu wasiokuwa waaminifu.‎

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *