Soko jipya la Kariakoo lililojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 28 limezinduliwa rasmi leo, likiwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 1,800. Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza upangishaji wa maeneo ndani ya soko hilo ufanyike kwa uwazi na haki, akisisitiza kwamba wafanyabiashara waliokuwepo awali wapewe kipaumbele.
Katika uzinduzi huo, Rais Samia ameuagiza uongozi wa soko kuhakikisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na matumizi inatumika ipasavyo ili kuondoa changamoto za kiutendaji zilizochangia matatizo yaliyosababisha soko hilo kuungua takribani miaka mitano iliyopita.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @rajjmsangi