Leo tarehe 13 Februari dunia inaadhimisha Siku ya Redio Duniani siku maalum ya kutambua mchango mkubwa wa redio katika maisha ya watu kote ulimwenguni Maadhimisho haya yalianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kuenzi redio kama chombo kinachowafikia watu wengi zaidi bila kujali hali ya kiuchumi au kijiografia.
Redio imeendelea kuwa njia rahisi nafuu na inayopatikana kwa watu wengi hususan katika maeneo ya vijijini ambako huduma ya intaneti bado ni changamoto. Tangu kuanzishwa kwake mwanzoni mwa karne ya ishirini redio imepitia mageuzi makubwa kutoka mfumo wa analogia hadi matumizi ya teknolojia ya kidijitali na utangazaji wa mtandaoni.
Leo redio si kifaa cha kusikilizia matangazo pekee bali ni jukwaa la mijadala elimu burudani na ushirikishwaji wa jamii. Kwa upande wa Tanzania historia ya redio ilianza rasmi mwaka 1951 kupitia Sauti ya Dar es Salaam ambayo baadaye ilikuja kuwa sehemu ya Shirika la Utangazaji Tanzania TBC .
Tangu wakati huo sekta ya redio imekua kwa kasi kubwa, hivi sasa kuna zaidi ya vituo mia mbili vya redio vilivyosajiliwa vikitoa huduma katika mikoa mbalimbali nchini Redio za jamii zimeongezeka na kusaidia kuwafikia wananchi katika maeneo ya pembezoni kwa lugha zao za asili. SOMA: Tanzania yaweka historia idadi ya redio, luninga
Ukuaji huu umechangiwa na kuongezeka kwa mahitaji ya habari elimu na burudani pamoja na maboresho ya teknolojia ya mawasiliano Takwimu zinaonesha kuwa sekta ya redio nchini inaendelea kukua kwa wastani wa zaidi ya asilimia nne kwa mwaka huku matumizi ya redio za mtandaoni yakiongezeka hasa miongoni mwa vijana
Katika maendeleo ya Tanzania, redio imekuwa na mchango mkubwa Kupitia vipindi vya elimu ya afya wakulima wamepata maarifa ya kilimo bora wananchi wameelimishwa kuhusu masuala ya afya kama chanjo na magonjwa ya mlipuko na jamii imewezeshwa kushiriki mijadala ya maendeleo Redio imekuwa daraja kati ya serikali na wananchi kwa kutoa taarifa za sera mipango na maamuzi muhimu ya kitaifa

Hata hivyo sekta ya redio inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo baadhi ya vituo hasa vya jamii vinakosa rasilimali fedha za kujiendesha kukabiliana na ushindani kutoka mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali umeathiri mapato ya matangazo na kuna haja ya kuwekeza zaidi katika vifaa vya kisasa na mafunzo kwa watangazaji
Teknolojia inaendelea kufungua fursa mpya kwa redio nchini Tanzania kwa lengo la kukidhi mahitaji ya utangazaji mtandaoni, programu za simu na mifumo mingine ya kidijitali yamerahisisha uzalishaji na usambazaji wa vipindi vya Redio na sasa zinaweza kuwafikia wasikilizaji popote walipo ndani na nje ya nchi kwa wakati mmoja
Tunapoadhimisha Siku ya Redio Duniani ni vyema kutambua kuwa redio bado ni sauti ya wengi na chombo muhimu cha maendeleo Endapo itaendelezwa kwa kuzingatia ubunifu maadili na matumizi sahihi ya teknolojia redio itaendelea kuwa mhimili muhimu wa maendeleo ya Tanzania kwa miaka mingi ijayo