Rais wa Marekani Donald Trump ametoa madai yanayohusisha ugonjwa wa usonjina matumizi ya chanjo ya utotoni na unywaji wa dawa maarufu ya maumivu ya Tylenol au Paracetamol kwa wanawake wajawazito. Katika mkutano usio wa kawaida katika Ikulu ya White House, Trump aliwashauri wamama wajawazito na wazazi wenye watato wadogo kutotumia dawa hiyo ya maumivu akipendekeza kuwa chanjo za kawaida zisitolewe kwa pamoja au katika miaka ya awali kwa mtoto. Ushauri kutoka kwa Trump, ambaye alikiri yeye si daktari, unakwenda kinyume na ule wa jamii za wataalamu wa matibabu, ambazo zinataja data kutoka kwenye tafiti nyingi zinazoonyesha kwamba dawa ya Tylenol, ni salama katika ustawi wa wanawake wajawazito. Makundi mengi ya utetezi wa matibabu, utafiti na usonji, ikiwa ni pamoja na Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Watoto na Chuo cha Madaktari wa Uzazi na Wanawake wamekanusha tangazo la rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *