Jamii, hususan wazazi, imehimizwa kuwa na utaratibu wa kuwachunguza watoto wao mara kwa mara ili kubaini mapema viashiria vya saratani, ugonjwa ambao si wa watu wazima pekee bali huweza hata kuwapata watoto wadogo.

Wito huo umetolewa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Saratani kwa Watoto Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka Februari 15, yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii na kuongeza uelewa kuhusu saratani kwa watoto.

Daktari Bingwa wa Watoto, Dkt. Dotto Aron, amesema siku hiyo ni muhimu katika kuhamasisha uelewa na kuchochea hatua za mapema za utambuzi na matibabu. Ameeleza kuwa wazazi wanapaswa kuwa makini kufuatilia mabadiliko yoyote yasiyo ya kawaida katika afya za watoto wao, ikiwemo uvimbe usioelezeka, homa za mara kwa mara, uchovu kupita kiasi au kupungua uzito bila sababu.

✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *