#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Paulo Chacha, ametangaza kuongeza dau la zawadi hadi kufikia Shilingi milioni 50 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa wa mauaji ya kinyama ya watoto wawili yaliyotokea mwaka 2022.
Mtuhumiwa huyo, anayefahamika kwa jina moja la Chacha, anasakwa kwa tuhuma za kuwaua watoto hao na kisha kuizika miili yao ndani ya nyumba yake katika kijiji cha Usimba, Wilaya ya Kaliua, kabla ya kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari, RC Chacha amesisitiza kuwa vyombo vya dola vinaendelea na msako mkali wa mtuhumiwa huyo ambaye amekuwa akikwepa mkono wa sheria kwa miaka minne sasa.
Ongezeko hilo la dau kutoka Shilingi milioni 20 za awali hadi milioni 50 ni mkakati wa serikali kuhamasisha wananchi kutoa taarifa siri zitakazosaidia kupatikana kwa mtuhumiwa huyo ili sheria ichukue mkondo wake na haki itendeke kwa wahanga wa tukio hilo la kusikitisha.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.