#HABARI:Mtumishi wa DAWASA Kibamba, alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo, kulipa faini ya kiasi cha Tshs. 1,000,000/= na kurejesha fedha kiasi cha Tshs. 297,000/= ambazo alizipokea kutoka kwa mlalamikaji, ikiwa ni fedha za rushwa ili arejeshe huduma ya maji aliyokuwa ameisitisha kwa kosa la kujiunganishia kinyume na taratibu (by pass).

Katika shauri hilo Na. 15649/2025, mshtakiwa Nsajigwa Dominico Mwaipyana ambaye ni Afisa Msaidizi DAWASA Kibamba, alishtakiwa kwa makosa mawili ya kuomba rushwa ya kiasi cha Tshs. 300,000/= na kupokea kiasi cha Tshs. 297,000/= kinyume na kifungu cha 15(1) (a), 2 na 3(b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA 329 R.E 2022, kutoka kwa mteja aliyesitishiwa huduma baada ya kujiunganishia maji hayo kinyume na taratibu.

Mshtakiwa alipatikana na hatia kwa makosa yote mawili na kuhukumiwa kilipa faini ya Tshs. 500,000/= kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kurejesha fedha kiasi cha Tshs. 297,000/= alizopokea.

Shauri hili liliendeshwa na wanasheria Khanifa Kapinga na Sophia Nyanda.

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *