HABARI: Wachimbaji madini wasiopungua 33 wamefariki dunia kutokana na uvujaji wa kaboni-monoksidi unaoshukiwa kutokea kwenye mgodi wa madini ya risasi na zinki katika Jimbo la Plateau katikati mwa Nigeria.
Mkasa huo umetokea kabla tu ya jua kuchomoza katika eneo lililo nje ya mji wa Wase linaloendeshwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Solid Unity Nigeria Ltd.
Gesi yenye sumu inaaminika ilikukusanyika chini ya ardhi katika handaki zisizo na hewa nzuri, na kusababisha wafanyakazi kuanguka kabla tu ya mwisho wa zamu yao ya usiku.
Waligunduliwa na wale waliokuwa wakiripoti kazini asubuhi, wachimbaji wengine zaidi ya 20 waliokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.