
Mwanamfalme wa zamani Andrew, ambaye anatimiza miaka 66 siku ya Alhamisi, amekamatwa kufuatia madai ya “utovu wa nidhamu katika utendaji wa majukumu rasmi,” polisi ya Windsor imetangaza, kuhusiana na tuhuma hizo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwanamfalme wa zamani wa Uingereza na kaka mdogo wa Mfalme Charles, Andrew Mountbatten Windsor, amekamatwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma huku polisi wakichunguza madai kwamba alishiriki habari za siri na Jeffrey Epstein aliyepatikana na hatia uhalifu wa kingono.
“Kama sehemu ya uchunguzi, sisi leo [Alhamisi, Februari 19] tumemkamata mtu mwenye umri wa miaka sitini kutoka Norfolk kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika majukumu yake ya umma, na kwa sasa tunafanya upekuzi katika anwani huko Berkshire na Norfolk. Mtu huyo kwa sasa yuko kizuizini,” kulingana na taarifa kutoka kwa Polisi ya Thames Valley.
“Sasa tumeanzisha uchunguzi kuhusu madai haya ya utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma,” amesema Naibu Mkuu wa Polisi Oliver Wright, aliyenukuliwa katika taarifa hiyo.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya hivi karibuni ya familia ya kifalme kwamba mmoja wa wanachama wake amekamatwa rasmi.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, amesema “hakuna mtu aliye juu ya sheria.”
Katika mahojiano kwenye BBC, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amemuomba Andrew Mountbatten-Windsor kutoa ushahidi, pamoja na “yeyote ambaye anaweza kuwa na taarifa ndogo zaidi,” katika kesi ya Epstein.
“Kila mtu ni sawa mbele ya sheria, hakuna aliye juu ya sheria. Na ni muhimu sana kwamba hili limhusu kila mtu bila ubaguzi,” Waziri Mkuu ameongeza, akimrejelea Andrew. Keir Starmer “hatapinga” ikiwa wabunge wanataka kujadili uhusiano kati ya Andrew na Epstein Bungeni.
Polisi kwa sasa wanachunguza madai kwamba mwanamke mmoja alikuwa mwathiriwa wa biashara haramu ya binadamu nchini Uingereza iliyofanywa na Jeffrey Epstein kwa niaba ya Prince Andrew, ambaye amekuwa akikanusha kila mara makosa yoyote.