HABARI: Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Thamini Uhai limezindua mradi wa Mjamzito na Mtoto Salama wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 12.15, unaolenga kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuboresha huduma za afya na kutoa kipaumbele kwa huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya miezi tisa na tiba kinga kwa akina mama wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai, Banzi Msumi amesema mradi huo wa miaka mitano utatekelezwa katika Mikoa ya Katavi, Geita na Kigoma kwa lengo la kuimarisha ubora wa huduma katika vituo vya afya hivyo kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.