Watuhumiwa watatu wamekamatwa katika Kata ya Lengijave mkoani Arusha wakidaiwa kuhusika na jaribio la kutorosha punda 21 kwenda nchi jirani bila kibali .
Tukio hilo limebainika Februari 20, 2026 kufuatia operesheni maalum iliyofanyika eneo hilo na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU) kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la ASPA. Watuhumiwa wanasubiri kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
#AzamTVupdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)