Mwanariadha wa Tanzania Gabriel Gerald Geay leo amefanikiwa kutetea taji la mbio za Marathon za Daegu China akitumia muda wa 2:08:11. Ushindi huo unaendana na kitita cha dola laki mbili(Shilingi milioni 517).
Mtanzania mwengine Emmanuel Daoudi Dinday alishika nafasi ya tatu akitumia muda wa 2:08:16 na kupata dola 45,000( 117,410,000 TZS ) huku nafasi ya pili ikishikwa na Chimdesa Debele Gudeta wa Ethiopia akitumia muda wa 2:08:08.
Gabriel mwaka jana alishinda mbio mbio hizo akitumia muda wa 2:05:20
#StarTvUPDATE
(Feed generated with FetchRSS)