#HABARI: Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeyapatia ufumbuzi malalamiko ya muda mrefu ya viwanja mbadala kwa wananchi wa Jiji la Dodoma.
Suluhisho hilo linafuatia malalamiko ya takribani wananchi 4000 wa Jiji la Dodoma wanaodai viwanja na Halmashauri ya jiji la Dodoma kuwapa ahadi bila kutekeleza mpaka sasa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo wakati akizungumza na wananchi wenye migogoro ya ardhi katika eneo la Mahomanyika lilopo kata ya Nzuguni jijini Dodoma.
Dkt Akwilapo amesema, eneo la Mahomanyika ni eneo la Serikali hivyo lipangwe na kupimwa kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya meneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma pamoja na matumizi ya Serikali.
Amesisitiza kuwa katika upangaji wa eneo hilo kipaumbele kiwe kutatua changamoto za wananchi wa jiji la Dodoma ambao kwa muda mrefu wamedai viwanja na jiji kuwaahidi bila ya kuwapatia.
Katika kufanikisha zoezi hilo, zimeundwa timu mbili kwa ajili ya upangaji na upimaji na pamoja na ile ya kushughulika na uhakiki wa wananchi wenye migogoro na kustahili kupatiwa viwanja mbadala.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)