#HABARI: Watu watano wamenusurika kifo baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Ajali hiyo ilihusisha gari la wagonjwa (Ambulance) la wilaya hiyo, lililokuwa likitokea Kijungu kuelekea Kibaya, pamoja na gari aina ya Noah lililokuwa likisafirisha abiria kutoka Kibaya kwenda Kijungu.
Kwa mujibu wa kiongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema zaidi ya watu watano walijeruhiwa katika ajali hiyo na wamepokelewa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu, ambapo majeruhi wengine wanapatiwa matibabu.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, huku uchunguzi ukiendelea kubaini kilichosababisha magari hayo kugongana.

(Feed generated with FetchRSS)