#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, huku akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia wilaya hiyo zaidi ya shilingi bilioni 317.

Katika taarifa hiyo iliyopitishwa kwa kishindo na Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, sekta ya barabara imeongoza kwa kutengewa shilingi bilioni 134, ikifuatiwa na sekta ya afya iliyopata shilingi bilioni 117 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika sekta ya elimu, jumla ya shilingi bilioni 57 zimetumika, huku wilaya ikijielekeza katika ujenzi wa shule za ghorofa zenye mifumo ya kisasa kama lifti na maabara katika kata za Vingunguti na Upanga.

Kwa upande wa afya, vituo vikubwa kama Mchikichini na Mzinga vimekamilika, huku mipango ikielekezwa katika ujenzi wa hospitali mpya zenye hadhi ya wilaya maeneo ya Mnazi Mmoja na Pugu ili kusogeza huduma bora karibu na wakazi wa Ilala.

Mhe. Mpogolo amebainisha kuwa ufanisi huo wa miradi ulichangia Ilala kuongoza kitaifa kwa kutoa kura milioni 1.2 katika uchaguzi mkuu uliopita.

Aidha, ameeleza kuwa wilaya imeongeza kiwango cha mikopo kwa wananchi kutoka asilimia 10 hadi 15, huku akiahidi kumaliza kero za migogoro ya ardhi na kutoa vitambulisho rasmi kwa wenyeviti wote wa serikali za mitaa ifikapo Machi mwaka huu.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *