Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba ametoa Sh1.8 milioni mkazi wa Arusha, Florah Mbeve amekabidhiwa Sh1.8 milioni ili akalipe deni alilomkopea mumewe kwenye Kikoba.

Hata hivyo, mara baada ya kumpatia fedha hizo mumewe huyo alitelekeza na kwa madai kuwa anazaa watoto wa kike pekee.

Mapema wiki hiiji 24, Florah aliwasilisha kero yake mbele ya Waziri Mkuu, Nchemba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo linapojengwa soko jipya la Kilombero wakati akiwa kwenye ziara ya siku tatu mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, alikuwa anauza vipande vya matikiti ili apate fedha za kujikimu na wanawe wanne na kiasi apeleke kwenye rejesho.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude ofisini kwake mbele ya Mwenyekiti wa kikundi cha Jikomboe,, Laurent Mwita Marwa.

Mkuu huyo amesema amemkabidhi kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Waziri Mkuu kama ambavyo aliahidi kwamba atampatia fedha hiyo ili kumuondolea adha na usumbufu alioupata kutokana na deni hilo analodaiwa kwenye kikoba.

Akizungumza baada ya kupokea fedha hizo, Marwa alishukuru kupewa rejesho la mama huyo kwa mkupuo kwa sababu tangu alipojifungua alikuwa hana chanzo cha uhakika cha fedha cha kuweza kurejesha mkopo wake.

Akitoa shukrani baada ya kukabidhiwa fedha hizo, Florah amemshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo kwa kuwa fedha hiyo amekuwa akidaiwa kwa muda mrefu na alishindwa kurejesha baada ya mumewe kumtelekeza yeye na watoto wake.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *