Siku moja baada ya rais wa Marekani kubadili ghafla msimamo wake wa kuishambulia Urusi na kuiunga mkono Ukraine, msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amesema kuwa “katika mahusiano yetu (kati ya Urusi na Marekani), njia moja inalenga kuondoa mambo yanayokera (…). Lakini mbinu hii inakwenda mwendo wa kinyonga. Matokeo yake yanakaribia sifuri.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kremlin pia imebanisha leo Jumatano, Septemba 24, kwamba Urusi haikuwa na chaguo ila kuendeleza mzozo wa kivita ulioanzishwa Februari 2022 na shambulio lake kubwa dhidi ya Ukraine

“Tunaendelea na operesheni yetu maalum ya kijeshi ili kuhakikisha maslahi yetu na kufikia malengo ambayo (…) rais wa nchi yetu ameanzisha tangu mwanzo. Na tunafanya hivi kwa sasa na siku za baadaye kwa nchi yetu, kwa vizazi vingi vijavyo. Kwa hiyo, hatuna njia nyingine,” ameongeza Dmitry Peskov.

Hivi karibuni Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa yuko tayari kuiwekea Urusi vikwazo vikali, lakini iwapo tu nchi za NATO zitatimiza baadhi ya masharti, ikiwa ni pamoja na kusitisha ununuzi wao wa mafuta ya Urusi.

Trump ametishia mara kwa mara Moscow kwa hatua kali zaidi, lakini hadi sasa hajachukua hatua yoyote mbele ya Kremlin kushindwa kufikia makataa yake na vitisho vya vikwazo.

Hapo awali Marekani iliweka ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa kutoka India, ikiwa ni pamoja na adhabu ya 25% kwa miamala na Urusi, chanzo kikuu cha ufadhili wa vita nchini Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *