
Marekani na Israeli, zimeendelea kueteleza mashambulio mazito nchini Iran, ambayo inasema haitarudi nyuma, katika vita hivyo ambayo haijafahamika vitamalizika lini.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati mashambulio hayo yakiendelea, Jeshi la kulinda mapinduzi ya Iran, limesema limekanusha ripoti za Marekani kuwa, ngome yake kuu ya makombora imeharibiwa vibaya, na kuongea kuwa bado ina silaha nzito na zenye nguvu.
Aidha, jeshi hilo limesema Iran haipo tayari kwa mazungumzo yoyote na Marekani, na kutishia kuzuia njia zote za kusafirisha mafuta kwenye ukanda wa Ghuba.
Nao wakaazi wa Iran wamesema mashambulio walioshuhudia siku ya Jumatatu usiku, yalikuwa ya kutisha, kulala kumekuwa kugumu na nyumba zao zimepatwa na nyufa.
Jeshi la Israel inalo limeanzisha mashambulio mapya siku ya Jumanne, yakilenga jiji kuu la Lebanon Beirut, katika mapambano dhidi ya kudndi la Hezbola.
