‎#HABARI: Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jafo, amewataka Watanzania kudumisha amani na mshikamano kama msingi mkuu wa maendeleo ya taifa.

Akizungumza kama mgeni rasmi katika mashindano ya 13 ya kuhifadhi Qur’aan Tukufu wilayani Kisarawe, Jafo amesisitiza kuwa Tanzania lazima iendelee kuwa kisiwa cha amani, hususan katika kipindi hiki ambacho mataifa mengine duniani yanakabiliwa na migogoro.

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu wilayani humo, Jafo amewahimiza wazazi na walezi kuwasimamia vijana wao ili wakue katika maadili mema na misingi imara ya dini.

Pia, ametoa rai kwa jamii kuwajali na kuwathamini walimu wa madrasa, akitambua mchango wao mkubwa katika kulea kizazi chenye nidhamu na kicho kwa Mungu.

Mashindano hayo yaliyoshirikisha watoto na vijana kutoka madrasa mbalimbali, yanalenga kukuza vipaji vya usomaji wa Qur’aan na kuimarisha mshikamano wa kijamii.

Jafo amebainisha kuwa malezi bora yanayopatikana kupitia mashindano hayo ni nyenzo muhimu katika kutengeneza raia wema watakaolinda tunu za taifa na kuchochea ustawi wa nchi kwa ujumla.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *