#HABARI: Wakazi na Wafanyabiashara wa mazao ya misitu katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma, wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa mikakati thabiti ya uhifadhi na ulinzi wa Maliasili.
Hata hivyo, wametoa mwito wa kuongezwa kwa kasi ya hamasa ya upandaji miti ili kukidhi mahitaji makubwa ya mazao ya misitu, hususan mbao, katika Kanda hiyo ya Kusini.
Akizungumza kuelekea Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa itakayofanyika Machi 21, mdau Zaid Hamduni na mkazi wa Mtwara, Said Ally, wameeleza umuhimu wa kuoanisha udhibiti wa misitu na jitihada za makusudi za upandaji miti mipya.
Wamesisitiza kuwa elimu zaidi inahitajika kwa jamii ili kuzuia uhaba wa maliasili hizo hapo baadaye.
Kwa upande wao, maafisa wa TFS Kanda ya Kusini, Lightness Chale na Dismas Mrwana, wamebainisha kuwa wakala huo unaendelea kudhibiti uvunaji holela na kusimamia taratibu za leseni kwa umakini.
Wameeleza kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha ulinzi wa misitu ya asili unakwenda sambamba na kutoa mwongozo wa kitaalamu kwa wananchi wanaotaka kuwekeza katika mashamba ya miti.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.