#HABARI: Katika kuimarisha mshikamano na mahusiano mema kazini, wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro wamekutana pamoja katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa chuoni hapo.
Baadhi ya watumishi walioshiriki katika hafla hiyo, wamesema kuwa tukio hilo limekuwa fursa muhimu ya kuwaleta pamoja wanajumuiya wa chuo na kuimarisha mshikamano.
Wamesema utaratibu huo wa kukutana katika matukio ya kijamii kama hayo, unachangia kujenga mahusiano mazuri kazini na kuimarisha mazingira ya kazi ndani ya taasisi.
Kupitia hafla hiyo, SUA imeendelea kudhihirisha umuhimu wa kukuza utamaduni wa umoja, kuheshimiana na mshikamano miongoni mwa wanajumuiya wake.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.