Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limefuta ushindi wa Senegal kama mabingwa wa taji la AFCON waliloshinda mwezi Januari, na kukabidhi ubingwa wa wapinzani wao Morroco ambao sasa ni mabingwa wa Afrika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika uamuzi  wa kushangaza, CAF imefuta ushindi wa  Senegal wa bao 1-0 iliyopata katika fainali ya michuano hiyo na badala yake kuipâ Morocco ambao walikuwa wenyeji wa michuano hiyo,  ushindi wa mezani wa mabao 3-0 na hivyo kutangazwa mabingwa wa taji la AFCON.

Bodi ya rufaa ya CAF imesema Senegal ilikiuka kanuni ya mchezo wa soka, baada ya wachezaji wake kususia mchezo huo na kuondoka uwanjani kabla ya kurejea tena, wakipinga maamuzi ya refarii kuipa Morocco penalti.

Des heurts ont éclaté dans les tribunes et au bord du terrain lors de la finale de la CAN 2025 à Rabat entre le Maroc et le Sénégal, le 18 janvier 2026.
Des heurts ont éclaté dans les tribunes et au bord du terrain lors de la finale de la CAN 2025 à Rabat entre le Maroc et le Sénégal, le 18 janvier 2026. AP – Youssef Loulidi

Uamuzi huu ambao unaingia katika histori ya soka la Afrika, umekuja baada ya Morocco kukata rufaa kupinga ushindi wa wa Senegal

Nchini Senegal, uamuzi huo umepokelewa kwa hasira kubwa, ambako Shirikisho la soka nchini humo, limesema uamuzi huo si wa haki, na kuongeza kuwa litakwenda katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo, kukata rufaa.

Aidha, wakuu wa mchezo wa soka nchini Senegal, wameulezea uamuzi wa kupokonywa ubingwa AFCON, kama kitendo kisichokubali na kinachoharibiu soka la Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *