
Ingawa imejikita sana katika vita vya Iran, Marekani inataka kuanzisha tena mazungumzo kuhusu mgogoro kati ya Rwanda na DRC. Ili kuwarudisha kwenye meza ya mazungumzo viongozi wa nchi hizo mbili, ambao misimamo yao imeendelea kutofautiana, mikutano kadhaa imeitishwa Washington katika siku za hivi karibuni, huku maandalizi yakiendelea kwa mkutano wa pande tatu uliopangwa kufanyika Jumatano, Machi 18.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Alipoulizwa kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya mashariki mwa DRC wiki moja iliyopita, Donald Trump alieleza kwa ufupi matumaini yake kwamba miji mikuu hiyo miwili “itazungumza hivi karibuni.”
Siku ya Jumanne, Machi 17, mikutano miwili ya pande mbili ilifanyika: mmoja kati ya wajumbe wa Kongo na Marekani, na mwingine kati ya wawakilishi wa Rwanda na Marekani. Kulingana na vyanzo kadhaa vya kidiplomasia, lengo kuu lilikuwa “kuandaa sehemu” na kujiandaa kwa mazungumzo yajayo.
Kuanzisha tena mazungumzo katika hali ya wasiwasi
Mpango huu unakuja katika muktadha nyeti sana, kwani unafanyika wiki mbili baada ya Marekani kuliwekea vikwazo jeshi la Rwanda na wiki moja baada ya kifo cha mfanyakazi wa misaada ya kibinadamu, raia wa Ufaransa, katika shambulio la ndege zisizo na rubani huko Goma.
Ingawa suala hili linachukuliwa kuwa nyeti, Marekani, katika hatua hii, imechagua kutohusisha Qatar au Umoja wa Ulaya katika juhudi zake. Lengo: kuepuka kutatanisha mambo na kusonga mbele haraka zaidi.
Hata hivyo, mkutano wa Jumatano leo, Machi 18, ambao ni kuzungumzia kuzinduliwa upya kidiplomasia na hali ya kijeshi katika mstari wa mbele, unaahidi kuwa mgumu, kwani misimamo ya wahusika wakuu wawili inaendelea kutofautiana. Wakati Kinshasa ikidai kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda, Kigali inajibu kwamba “sio suala la kufurahia faida na pia kumtaka anayefanya upate faida hiyo” na inaishutumu DRC kwa kuendelea kushirikiana na FDLR ili kuhatarisaha usalama wa Rwanda, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.
Washington, kwa upande wake, inakusudia kutumia fursa hiyo kuwasilisha ujumbe wake yenyewe. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyotangazwa katika hatua hii isipokuwa mkutano huo utoe “uamuzi halisi” ambao unaweza kufufua mchakato wa amani, chanzo cha kidiplomasia kinaeleza.