
Je, MINUSCA inafunga shughuli zake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, au huu ni mpangilio mpya wa kimkakati wa shughuli zake nchini humo? Swali hili limechochea mjadala na wasiwasi miongoni mwa wakazi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa wiki kadhaa.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Bangui, Rolf Steve Domia-Leu
Kote nchini, vituo vingi vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa vinafunga milango yao hatua kwa hatua, wakati mwingine baada ya zaidi ya miaka kumi ya uwepo wake endelevu. Kama ukumbusho, MINUSCA ilitumwa mwaka wa 2014 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika muktadha wa mgogoro mkubwa kufuatia mapinduzi ya Machi 24, 2013. Kutokana na uvumi unaoendelea wa kuondoka moja kwa moja kwa MINUSCA, ujumbe huo umelazimika kujibu. Wakati wa mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari siku ya Jumatano, ilikanusha rasmi nia yoyote ya kuondoka, badala yake ikirejelea mpangilio mpya wa kutumwa kwake.
Katika maeneo kadhaa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yaambapo vituo vya MINUSCA vilinekana kusitisha shughuli zao, wakazi wanao hofu ya kurudi kwa ukosefu wa usalama ambao hapo awali ulidhibitiwa kutokana na uwepo wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Mnamo Machi 19, kambi ya Dékoa ilifungwa rasmi, na kuashiria hatua mpya katika mchakato huu.
Kwa wakazi wengi, uamuzi huu umechochea hofu ya kuibuka tena kwa makundi yenye silaha. “Sasa tunaogopa kulengwa na mashambulizi na unyanyasaji. Je, tutaweza kwenda kwenye mashamba yetu, kusafiri kwenye barabara za vijijini, au kufanya biashara?” anauliza Suzanne, mkazi wa moja ya maeneo husika.
Kwa upande wake, MINUSCA inataja vikwazo vikubwa vya kifedha. Kulingana na Kamanda wa Jeshi, Humphrey Nyone, misheni hiyo inapanga kufunga jumla ya vituo 21 ifikapo mwisho wa mwezi Machi 2026. Hata hivyo, alifafanua kwamba vituo vingi hivi vilikuwa vya muda na kwamba kufungwa kwake hakumaanishi kuondolewa kwa wanajeshi au kutelekezwa kwa raia.
Kambi zilizofungwa sasa zimekabidhiwa kwa mamlaka za Jamhuri ya Afrika ya Kati na Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambavyo vina jukumu kubwa la usalama nchini.
Ujumbe huu wa uhakikisho pia uliwasilishwa na msemaji wa ujumbe huo, Florence Marshall, ambaye alibainisha: “Upangaji huu upya si kujiondoa kwa moja kwa moja kwa MUNISCA nchini. Uamuzi kama huo,” alirudia, “uko chini ya mamlaka ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pekee.”