Vijana mkoani Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika maeneo yao ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga, Ramadhan Ally Omary, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana waliokusudiwa kuwa wakufunzi katika wilaya zao.
Amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa vijana, hivyo wanapaswa kuacha malalamiko na kutumia fursa zilizopo kujipatia kipato. Ameongeza kuwa mafunzo hayo yataendelea katika ngazi za halmashauri, na baada ya hapo vitaundwa vikundi vitakavyopatiwa mikopo kusaidia kutimiza ndoto zao.
(Feed generated with FetchRSS)