Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali jinai za adui za kuvishambulia vyuo viku na vituo vya elimu nchini Iran.

Ismail Baqaei ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kufuatia jinai za adui, Marekani na Mzayuni, za kuvishambulia vyuo vikuu na vituo vya elimu na utafiti nchini Iran kwamba: Wavamizi hawa kila siku wanaweka wazi zaidi lengo lao halisi la vita hivi; mashambulizi dhidi ya vyuo vikuu yanadhihirisha chuki ya adui kwa maendeleo ya kisayasnsi ya Wairani.

Baqaei ameeleza kuwa: Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Isfahan na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Tehran ni vyuo vikuu viwili tu kati ya makumi ya vyuo vikuu na vituo vya utafiti vilivyoshambuliwa katika siku 30 zilizopita katika vita vya wavamizi dhidi ya taifa la Iran na kwamba kitendo cha adui huyu, kama vitendo vingine vya kukata tamaa, hakitaufika popote, kwa sababu sayansi na maarifa ya Iran si jambo linaloingizwa kutoka nje, bali ni mtaji na uwekezaji wa kudumu na endelevu wa ustaarabu halisi ambao umekuwa ukinufaisha jamii ya binadamu kutokana na mafanikio yake.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa: Kile walichokitaja kama sababu ya shambulio hilo la kijeshi, chini ya kichwa cha habari “mpango wa nyuklia” na “tishio linalokaribia”, si kitu kingine zaidi ya visingizio vya kipuuzi na vya kubuni ili kuficha nia zao halisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *