Rosatom inaendelea kupanua shughuli zake za madini kimataifa kupitia ushirikiano mpya na Brazil, kwa kuanzisha kampuni ya pamoja itakayoshughulika na utafiti na uendelezaji wa madini muhimu kwa teknolojia za kisasa. Makubaliano hayo yalisainiwa katika mkutano wa Nuclear Summit 2026 uliofanyika Rio de Janeiro, yakilenga utafiti wa kijiolojia, upatikanaji wa leseni na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya uchimbaji.

Kwa Tanzania, hatua hii inaashiria fursa mpya. Kupitia kampuni tanzu ya Mantra Tanzania, Rosatom tayari inaendeleza utafiti wa urani, hatua inayoweza kufungua uwekezaji zaidi, uhamishaji wa teknolojia na kuboresha sekta ya madini nchini.

Ushirikiano huu unaakisi mwenendo wa kimataifa ambapo mahitaji ya madini ya kimkakati yanaongezeka, na nchi kama Tanzania zina nafasi ya kunufaika endapo rasilimali zitasimamiwa kwa uendelevu na kuleta manufaa ya kiuchumi kwa wananchi.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *