Vibanda vya wafanyabishara eneo la Mawasiliano Jijini Dar es Salaam vimeteketea kwa moto.
Inaelezwa kuwa moto huo umeibuka ghafla leo
jioni na kuteketeza baadhi ya vibanda hivyo vilivyo katika eneo hiilo.
Hata hivyo, chanzo cha moto huo hakijafahamika mara moja.
Vikosi vya uokoaji kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wanachi wameonekana wakipambana kuzima moto huo uliodumu kwa saa kadhaa.
*Star TV Digital unatoa pole kwa wafanyabiashara wote waliokumbwa na janga hilo. Endelea kufuatia taarifa zaidi kupitia kurasa za Star TV Digital.*
(Feed generated with FetchRSS)