#HABARI: Serikali ya Tanzania imeelezea mafanikio yake katika maendeleo ya miji na sekta ya makazi wakati wa Kongamano la Pili la Miji Africa (2nd African Urban Forum), linalofanyika jijini Nairobi, huku ikitoa wito kwa wawekezaji wa ndani na kimataifa kuchangamkia fursa zilizopo nchini humo.

Hayo yameelezwa jijini Nairobi nchini Kenya na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo, wakati akitoa tamko la Tanzania kuelezea jitihada za Serikali katika kuchochea maendeleo endelevu ya miji na makazi, ikiwa ni pamoja na sera, mipango na mikakati inayotekelezwa kuboresha makazi na upangaji wa miji.

Amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Ajenda 2063 ya Umoja wa Africa, hasa katika maeneo ya miundombinu, upatikanaji wa nishati, utoaji wa huduma za kijamii na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Mhe. Dkt Akwilapo ameelezea pia mikakati ya serikali ya Tanzania katika kukabiliana na changamoto za ukuaji wa kasi wa miji pamoja na upungufu wa makazi, ambapo kwa sasa makazi yasiyo rasmi yanakadiriwa kufikia asilimia 67.3.

Amesema, katika kukabiliana na hali hiyo, serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza mageuzi ya sera, kuanzisha mifumo bunifu ya fedha, kuboresha umiliki wa ardhi pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika makazi nafuu kupitia ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi.

Kongamano la Pili la Miji Africa limezinduliwa rasmi na Rais wa Kenya Mhe. William Ruto na linaongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Adequate Housing for All Advancing Socio-Economic and Environmental Transformation Towards the Realization of Agenda 2063’ ikilenga kuhamasisha mijadala inayotoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu na suluhisho bunifu katika kukabiliana na changamoto za maendeleo ya miji na makazi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *