Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kimesema huduma za usafiri zitaendelea kutolewa kama kawaida kufuatia mazungumzo yaliyofanyika kati yao na serikali.
Katibu Mkuu wa TABOA, Priscus John amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya pande zote kufikia muafaka, na hivyo kusitisha tamko la awali la kusimamisha huduma ifikapo Aprili 12 endapo nauli zisingepandishwa. Aidha, amewataka watoa huduma kuendelea na shughuli zao huku serikali ikiendelea kushughulikia changamoto zilizopo.
#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)