Mtaalamu wa saikolojia, John Ambrose, ameitaka serikali kupitia wabunge kutunga sheria maalum za kuwasaidia watoto wenye changamoto ya akili.

Ambrose amesema watoto hao wanakabiliwa na mazingira magumu, huku walezi wao wakihitaji msaada zaidi kutoka kwa jamii ili kuwahudumia ipasavyo.

Amesisitiza kuwa kundi hilo linahitaji uangalizi maalum ili liweze kuishi maisha bora kama wengine.

Katika kuhamasisha hatua, Ambrose ametangaza kuanza yeye kwa kutoa mfuko mmoja wa saruji kwa kila mbunge, akilenga kuwachochea wabunge kushiriki katika kusaidia watoto hao.

✍Ibrahimu Kilumbo
@elesia_haule

#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *