Mbunge wa Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa, ameishauri serikali kuweka utaratibu wa kuwa na akiba ya dizeli, sawa na ilivyo kwa dhahabu, ili kulinda uchumi dhidi ya misukosuko ya upatikanaji wa nishati.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni Dodoma, Kadogosa amesema uhaba wa mafuta umekuwa ukijirudia na unaweza kuathiri utekelezaji wa malengo ya uchumi, ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Amesema serikali pia inapaswa kuwekeza katika matumizi ya nishati mbadala, ikiwemo kuhamasisha mabasi ya usafiri wa umma kutumia gesi na kuweka miundombinu ya magari ya umeme kwa taasisi za serikali.
Ameonya kuwa bila mipango ya muda mrefu, changamoto ya upatikanaji wa mafuta itaendelea kujitokeza na kuathiri uchumi.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)