Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance,ameishutumu serikali ya Iran kwa kujihusisha na “kitendo cha ugaidi wa kiuchumi” kwa kuzuia usafiri kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz.
Vance amemwambia Brett Baier wa Fox News kuwa Rais Donald Trump ameonyesha kwamba “wote wawili wanaweza kucheza mchezo huo”.
Anasema ikiwa Wairani “watajihusisha na ugaidi wa kiuchumi”, basi Marekani itazingatia kanuni kwamba “hakuna meli za Iran zitakazoruhusiwa kutoka katika mlango bahari wa Hormuz”.
Vance pia amezungumzia mazungumzo na Iran yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, akisema kuwa maendeleo makubwa yamepatikana.
“Mpira uko upande wa Iran,” amesema.
Makamu huyo wa rais wa Marekani pia Iametaja kuwa ran inapaswa kuwa tayari kubadilika na kukubali “mambo muhimu” yanayodaiwa na Marekani, udhibiti wa Marekani juu ya urani uliyorutubishwa wa Iran, pamoja na utaratibu wa uthibitishaji ili kuhakikisha kuwa haujatengeneza silaha ya nyuklia.
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)