Mbunge wa Busega, Simon Songe ameomba serikali kuingilia kati utaratibu unaolalamikiwa na wakulima wa pamba mkoani Simiyu, unaowalazimisha kuuza mazao yao kwa mnunuzi mmoja.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni Dodoma, mbunge huyo amesema Simiyu inachangia takribani asilimia 51 ya uzalishaji wa pamba nchini, lakini wakulima wanakabiliwa na masharti ya wawekezaji yanayodai kuwalazimisha kuuza pamba kwa mtu mmoja aliyepo eneo husika.

Amesema utaratibu huo unarudisha nyuma mfumo wa ushindani wa soko huria na umekuwa ukilalamikiwa na wakulima.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *