
Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Ijumaa jioni kwamba kizuizi cha kijeshi kitaendelea kwenye bandari za Iran ikiwa hakuna makubaliano ya amani yatakayofikiwa na Tehran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Marekani Donald Trump amesema “kizuizi cha kijeshi kitaendelea kutekelezwa kwa nguvu zote, hadi pale tutaafikiana na Iran kwa 100%”, akiongeza kwamba huenda asiongeze muda wa kusitisha mapigano baada ya kumalizika siku ya Jumatano. Iran, kwa upande wake, ilitishia leo Jumamosi kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz ikiwa Marekani itaendelea kuzingirwa kwa bandari za Iran, baada ya kutangaza siku iliyopita kufunguliwa tena mlango huo kwa meli za kibiashara.
Rais huyo pia amesema kuwa mchakato huo unatarajiwa kufanyika haraka kwa kuwa sehemu kubwa ya masuala tata tayari yamejadiliwa.
“Mchakato huu unapaswa kwenda haraka sana kwa kuwa sehemu kubwa ya vipengele vya mkataba wa makubaliano yameafikiwa. Asanteni kwa kuzingatia jambo hili” alisema Trump
Wakati huo huo Trump amesema kwamba uranium iliyorutubishwa iliyohifadhiwa na Iran “itasafirishwa Marekani,” muda mfupi baada ya Tehran kutangaza kwamba “haitahamishiwa popote.