Serikali imesema kufikia Machi 2026 nchi imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme na kufikia megawati 4,522.54 kutoka megawati 4,031.71 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.17 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2025.

Akitoa takwimu za uzalishaji, usambazaji na matumizi ya umeme nchini, Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema mbali ya ongezeko la uzalishaji serikali pia imeongeza uwezo wa usafirishaji wa umeme pamoja na watumiaji wa nishati hiyo nchini katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *