Takribani wakazi 29,000 kutoka wilaya za Ilala, Temeke, Kigamboni, Ubungo, Kinondoni na Bagamoyo mkoani Pwani wanatarajia kunufaika na huduma za maji baada ya miradi sita mikubwa ya majisafi na salama yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.586 kukaguliwa na Mio za Mwenge wa Uhuru kabla ya kuhitimishwa kwake kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Miradi ya majisafi iliyotembelewa na kuridhiwa ni mradi wa kisima cha maji Ilala Kota wilayani Ilala unaogharimu Shilingi milioni 164 huku ukitarajia kugusa maisha ya wakazi 2,640.
Miradi mingine ambayo itakayowagusa wakazi wa Dar es Salaam ni mradi wa maji Kiziza uliopo wilaya ya Kigamboni, mradi wa wa bilioni 1.82 wa Msumi utakaonufaisha wakazi 18,000, mradi wa kisima cha maji Makangarawe wilayani Temeke uliogharimu milioni 190 na unaowalenga wakazi 2,000 na mradi wa kisima cha maji Kituo cha Afya Kinondoni uliogharimu milioni 191.7 na unalenga kuwanufaisha wakazi 3,360.
Mradi mwingine ambao umeugusa mkoa wa Pwani ni mradi wa maji Kibosha Mnarani wilayani Bagamoyo uliogharimu milioni 182.5.
Kufuatia kukubaliwa kwa miradi hiyo na mbio za Mwenge wa Uhuru, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amesema kuwa wanaendelea kusimamia maagizo ya Rais Samia ya kuhakikisha huduma hii muhimu ya maji inapatikana muda wote katika maeneo yote pasipo na usumbufu.
Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)