Israeli na Lebanon zinatarajia leo Alhamisi, Aprili 23, kuanza tena mazungumzo huko Washington, chini ya upatanishi wa Marekani, karibu wiki moja baada ya pande hizo mbili kukubaliana kusitisha mapigano kwa siku kumi. Tangu wakati huo, jeshi la Israel na kundi la Lebanon lenye silaha la Hezbollah wameendelea kushambuliana. Lakini Ikulu ya White House imeelezea nia yake ya kufikia makubaliano kamili ya amani kati ya Israel na Lebanon.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Duru mpya ya mazungumzo kati ya Lebanon na Israel itafanyika leo Alhamisi, Aprili 23, nchini Marekani, amethibitisha Rais wa Lebanon Joseph Aoun. Lebanon inakusudia kuomba kuongezwa kwa mwezi mmoja kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Wakati mvutano ukiongezeka kati ya Tehran na Washington, licha ya kuongezwa kwa muda wa kusitisha mapigano, matarajio ya duru ya pili ya mazungumzo yanaahirishwa kila siku. Hata hivyo, huko Islamabad, kila kitu kiko tayari kuwapokea wajumbe, na athari kubwa kwa maisha ya wakazi, ambao wana nia ya hali hiyo kutatuliwa.

Huko Islamabad, maisha yamesimama kwa siku kadhaa: barabara kuu zimezuiwa, usafiri wa umma umesitishwa, na karibu hakuna kitu na hakuna mtu anayeingia au kutoka katika mji mkuu, ambao uko chini ya ulinzi mkali. Maelfu ya maafisa wa polisi na wanajeshi wametumwa maeneo mbalimbali ya mji mkuu, anaripoti mwandishi wetu huko Islamabad, Ondine de Gaulle.

Kwa sababu hiyo, wakazi wa mji mkuu wahasafiri kwa urahisi, watumishi wa umma na wafanyakazi wa ofisi wameombwa kufanya kazi wakiwa nyumbani, na wafanyakazi wengi wamepoteza kazi zao. Uchumi mzima umezorota.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *